Madrid yakabwa koo na Las Palmas zafungana 3-3


Timu ya Real Madrid imeshindwa kufurukuta mbele ya Las Palmas baada ya kutoka sare ya bao 3-3 katika uwanja wa Santiago Bernabeu.

Real Madrid ilipata bao la kuongoza kupitia Isco aliyefunga dakika ya 8 hata hivyo kiungo wa Las Palmas Tana alichomoa bao dakika ya 10.

Kipindi cha pili Las Palmas walipata bao na kuyafanya matokeo kuwa 3-1, lakini Christiano Ronaldo alichomoa bao hizo na matokeo kuwa 3-3.

Pia katika mchezo huo mshambuliaji wa kimataifa wa Wales Gareth Bale alitolewa nje ya uwanja baada ya kuoneshwa kadi nyekundu na mwamuzi katika dakika ya 47 ya mechi hiyo.

Comments