Timu ya Manchester united itakuwa na kibarua cha kuwakabiri mahasimu wao chelsea bila washambuliaji wao muhimu.
Man utd itawakosa Zlatan Ibrahimovic ambaye amefungiwa mechi tatu, Wayne Rooney na Rashford ambao hawapo fiti kiafya.
Mechi hiyo ambayo ipo kwenye hatua ya robo fainali ya kombe la FA itachezwa katika uwanja wa Stamford Bridge jijini London.

Comments
Post a Comment