Mshambuliaji wa Monaco Kylian Mbappe ameziweka vitani klabu kubwa zinazotamba barani Ulaya.
Raia huyo wa Ufaransa ndiye habari ya mjini kwa sasa kutokana na uwezo wake mkubwa wa kufumania nyavu na kusakata kabumbu uwanjani.
Mbappe mwenye miaka 19 anawindwa na timu kubwa barani Ulaya ikiwemo Barcelona, Real Madrid, Man city na Man utd ambao wote kwa pamoja wametangaza nia ya kumsajili nyota huyo.
Mbappe amefunga bao 10 katika mechi 10 za mwisho na kuingoza Monaco kuindoa city kwenye hatua ya 16 bora.

Comments
Post a Comment