Messi ainyanyua Argentina Kombe la dunia


Nyota wa Barcelona Lionel Messi amefufua matumaini ya taifa la Argentina baada ya kufunga bao pekee la ushindi dhidi ya Chile.

Messi alifunga bao hilo kwa mkwaju wa penati kunako dakika ya 16 ya mechi hiyo baada ya Angel Di Maria kufanyiwa madhambi katika eneo la 18.

Ushindi huo unaifanya Argentina kusonga mbele hadi nafasi ya 3 ya msimamo kati ya timu 10 zinazowania kufuzu kombe la dunia baada ya kukusanya jumla ya pointi 22 katika mechi  13.

Mbali na mechi hiyo, timu ya Brazil imeigalagaza Uruguay kwa kipigo cha Bao 4-1, ambapo kiungo wa zamani wa Tottenham Paulinho alifunga hat trick na lingine liliwekwa nyavuni na Neymar.

Comments