Klabu ya Yanga imemziba mdomo msemaji wa Ruvu Shooting Masau Bwire baada ya kuifunga timu hiyo bao 2-0.
Awali kabla ya mchezo huo msemaji huyo alitamba kuizika Yanga baada ya kupokea kipigo cha bao 2-1 kutoka kwa Simba.
Msuva alianza kuifungia bao la kwanza dakika dakika ya 27 na Emanuel Martin alishindilia ushindi huo baada ya kutupia bao la pili katika dakika ya 90 akiunganisha krosi safi ya Simon Msuva.
Ushindi huo umeiongoza Yanga kuifukuzia Simba yenye pointi 54 zikiwa zimesalia pointi mbili zote zikiwa zimecheza michezo 23.

Comments
Post a Comment