Naby Keita, Lacazzete kutua Liverpool?


Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp ameazimia kuimarisha kikosi cha Liverpool baada ya kuweka mezani jina Naby Keita na Alexander Lacazzete.

Naby Keita ni Raia wa Guinea ambaye anafanya vema katika timu ya RB Liepzing na ambayo inafanya vizuri katika ligi ya Bundesliga.

Bado kuna mapungufu kiasi katika safu ya kiungo ya Liverpool na Klopp anataka kuiimarisha zaidi kutokana na timu yake kusua sua licha kutandaza soka bora uwanjani.

Kwa upande mwingine Klopp harizishwi na safu ya ushambuliaji kwenye timu yake na ambayo imeegemea zaidi kwa Sadio Mane na sasa anajipanga kumsajili Lacazzete kutoka Olympic Lyon ya Ufaransa.

Bila shaka Firmino amechemsha kuyabeba ipasavyo majukumu ya kufunga magoli uwanjani, na hili limeonekana wazi msimu huu.

Liverpool inahitaji mshambuliaji wa kiwago cha daraja la kwanza ambaye ataweza kupambana katika mazingira yoyote yale.

Jambo hili linaonekana kuigharimu Liverpool msimu huu licha ya kuwa wanakosa ukuta imara katika eneo la ulinzi lakini ni wazi kuwa strika ikiwa bora pia husaidia kufuta makosa.

Taratibu anaona ni namna anaweza kuwa na Liverpool bora msimu ujao. Huenda Lacazzate akachukua nafasi ya kwanza ya kusajiliwa kwenye timu hiyo.

Sturridge ambaye alikuwa tumaini la timu hiyo kwa sasa amekuwa mwenye  kuandamwa na majeraha mara kwa mara na hii imepunguza kasi na ufanisi wake uwanjani.

Ingawa Klopp anatamani kumwachia Sturridge ambaye anaonekana wazi kuchoshwa na maisha ya Anfield lakini anasita kulingana na Hali ya kikosi ilivyo.

Endapo Klopp atafanikiwa kushusha strika wa maana Anfield huenda akamaliza matatizo yanayo muandama kikosini nadhani pia atafanikiwa kuachana na Sturridge.

Tutegemee mabadiliko katika safu ya kiungo na safu ya ushambuliaji ya Liverpool. Huenda Liverpool ikavunja kibubu rasmi kwa kufanya usajili wa maana kama klabu zingine ulimwenguni.

Sitashangaa endapo Naby Keita na Lacazzete watatua Liverpool katika kipindi cha majira ya joto.

Comments