Leo jioni katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kutakuwa na mtanange mkali kati ya Yanga na Azam.
Haijulikani nani atakuwa mbabe katika mechi hiyo, ingawa Yanga itawakosa nyoka wake muhimu kama Amis Tambwe na Donald Ngoma.
Kwa upande wa Azam inaonekana kuwa na kikosi imara kiasi ingawa inaweza kumkosa Aggrey Morris ambaye alianza mazoezi ndani ya wiki baada ya kupona jeraha la mfupa wa paja.
Azam na Yanga wamekuwa na mfululizo wa matokeo ya sare kila wanapokutana kwenye mechi za ligi kuu Tanzania Bara, hu ukiwa ni msimu wa nne hakuna aliyewahi kutoka na pointi 3.
Kwa upande wa Yanga Simon HappyGod Msuva na Obrey Chirwa ndiyo watakaoongoza safu ya ushambuliaji wa timu hiyo, Geoffrey Mwashiuya na Emanuel Martin wanaonekana kuwa fiti pia.
Safu ya ushambuliaji ya Azam pia haina mapungufu sana, ingawa haitashangaza endapo John Bocco 'Adebayor' ataukosa mchezo huo.

Comments
Post a Comment