Aliyekuwa kocha na mkurugenzi wa benchi la ufundi kwenye klabu ya Yanga Hans Pluijm huenda akatua Singida united muda wowote kuanzia sasa.
Baadhi ya taarifa zilizagaa kwenye kurasa za mitandao ya jamii zikimuonesha kocha huyo akiwa kwenye picha ya pamoja na mchezaji mpya aliyesaini kwenye timu hiyo akitokea Zimbabwe.
Singida United ambayo imepanda daraja kuelekea ligi kuu ya Vodacom tayari imeanza kufanya mageuzi ikiwemo mchakakato mzima wa kukamilisha dili la Pluiijm.
Hata hivyo Pluijm alikanusha taarifa za yeye kusaini kwenye timu na kusisitiza kuwa bado wapo kwenye hatua ya mazumgumzo.
"Hakuna ukweli kuwa nimesaini, bado nipo kwenye mazungumzo na Uongozi wa timu endapo nitasaini kila kitu kitakuwa wazi." Alisema Pluijm.

Comments
Post a Comment