Timu ya Singida united imezidi kuongeza ubora wa kikosi chake kitachoshiriki ligi kuu Tanzania Bara baada ya kusajili nyota wengine wawili kutoka Zimbabwe.
Nyota hao ni Elisha Muroiwa mwenye miaka 27 na Wisdom Mutasa mwenye umri wa miaka 22.
Hii ni Salamu ya Hans Pluijm kwa timu za za Simba, Yanga na Azam ambazo ambao kwa sasa ndiyo wababe wa ligi kuu Vodacom.
Licha ya kusajili Raia watatu kutoka Zimbabwe bado timu hiyo chini ya Pluijm imeendelea kufanya mikakati mizito ya usajili kwa ajili ya kufanya kwenye msimu mpya wa ligi kuu 2017/18.

Comments
Post a Comment