Kocha wa sasa wa Barcelona Luis Enrique amesema kuwa ataacha na klabu hiyo mwishoni mwa msimu.
Enrique ambaye mkataba wake umalizika June mwaka huu alisema kuwa hataongeza mkataba mpya na timu hiyo kwa kuwa anahitaji kupumzika kwa sasa.
"Ni uamuazi mgumu lakini natangaza kuachana na Barcelona, mkataba wangu utafikia tamati mwezi June mwaka huu.
"Sababu kuu nahitaji kupumzika kwa sasa baada ya kumaliza miaka 3 nikiwa na Barcelona." Alisema Enrique
Wiki mbili zilizopita kocha huyo alikuwa kwenye wakati mgumu baada ya Barcelona kuchezea kichapo cha bao 4-0 kutoka kwa PSG.
Enrique mwenye miaka 46 ameingoza Barca kutwaa taji la ligi kuu mara 2, klabu bingwa Ulaya mara 1 na Copa del mara 2 na tayari Barcelona imetinga fainali na taji na klabu ya Alaves.

Comments
Post a Comment