Real Madrid kusajili wawili Chelsea


Timu ya Real Madrid inajiandaa kumwaga mpunga mrefu ili kuwanasa nyota wa Chelsea Mshambuliaji Eden Hazard na golikipa Thibaut Courtois .

Hazard amekuwa akiivutia Real Madrid kwa muda mrefu kutokana na kiwango bora ambacho kimeinyanyua Chelsea wakati wote.

Aidha timu hiyo bado imeendelea kusaka mbadala wa kipa wa sasa Navas ambaye amekuwa na kiwango cha kawaida ikilinganishwa na ule uwezo wa Iker Casillas.

Real Madrid inaona golikipa wa Chelsea Thibaut Courtois ndiye mchezaji sahihi wa kuchukua nafasi ya Navas pale Bernabeu.

Ingawa kiasi hicho hakijawekwa wazi, huenda wababe hao wa Santiago Bernabeu wakatoa kiasi kikubwa cha fedha ili kuishawishi Chelsea kuwaachia nyota hao.

Comments