Samatta kuikosa Burundi leo.


Kikosi cha timu ya Taifa kinachonolewa na kocha Salum Mayanga kitashuka dimbani kuivaa Burundi bila nahodha wao Mbwana Samatta.

Nafasi ya Samatta itajazwa na Farid Mussa ambaye kwa anakipiga katika timu ya Deportivo Tenerife inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Spaini.

Mayanga amemruhusu Mbwana Samatta kutimka ikiwa pia ni sehemu ya kujaribu kikosi chake cha ndani kwa ajili ya michuano ya CAN ambayo hushirikisha wachezaji wa ndani.

Mayanga alianza vizuri katika mchezo wa kwanza ambapo aliweza kutoka kifua mbele baada ya kuifunga Botswana bao 2-0.

Comments