Simba yaipa jeuri Mbeya City


Baada ya kumbana mnyama katika uwanja wa Taifa hatimaye Mbeya city imesema kuwa kwa sasa wana morali ya kushinda kila mechi.

Mbeya city walitoka sare ya bao 2-2 na Simba ambayo ilirazimika kutafuta matokeo ya sare kutokana kiwango kikubwa ambacho Mbeya city ilikionesha.

Kocha wa timu hiyo Kina Phiri alisema kuwa wamejipanga kupata ushindi katika kila mechi kutokana na hali ya wachezaji kuongezeka.

"Baada ya matokeo tuliyopata dhidi ya Simba morali ya wachezaji imeongezeka na sasa tuna imani ya kushinda kia mechi.

"Kuna mabadiliko makubwa kikosini, tuna imani tutamaliza vizuri mechi zetu zilizobaki."  Alisema Phiri .

Comments