Simba yakabwa koo na Mbeya city


Klabu ya Simba imeshindwa kuendelea na mbio za ushindi baada ya kutoka sare ya bao 2-2 na Mbeya city katika uwanjani wa taifa.

Mbeya city ilianza kupata bao la kuongoza kupitia Bitram Nchimbi, na Simba ilichomoa bao hilo kupitia Ibrahim Ajib aliyefunga kwa mkwaju wa freekick.

Licha ya Simba kushambulia kwa nguvu baada ya kuchomoa bao, Mbeya city iliweza kuongeza bao la pili kupitia Kane Ally hata hivyo Shinza kichuya aliokoa wanamsimbazi hao baada ya kuchomoa kwa mkwaju wa Penati.

Hadi mwamuzi anapuliza kipenga cha kuhitimisha mchezo huo matokeo ya mwisho yalikuwa 2-2.

Comments