Ukata wamwondoa Pluijm Yanga


Aliyekuwa kocha wa zamani wa klabu ya Yanga Hans Van Der Pluijm ameondolewa rasmi mwenye nafasi yake ya ukurugenzi.

Awali nafasi ya kocha huyo ilichukuliwa na mzambia George Lwandamina na kupewa nafasi mpya kama mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo.

Imeelezwa kuwa hali ya kiuchumi haiko vizuri kwenye timu hiyo na hivyo wamelazimika kumwondoa Pluijm kutokana na uhaba wa pesa.

Tangu alipotiwa kizuizini mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuph Manji wababe hao wa jangwani wameingia kwenye misuko suko ya kifedha.

Comments