Timu ya Manchester united imeingia kwenye mipango ya kumnasa mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez.
Sanchez alitangaza kuachana na Arsenal na kurejea Hispania kwa mara nyingine ambapo anahusishwa na timu ya Sevilla.
Raia huyo wa Chile amebadili mtazamo wa kocha Jose Mourinho ambaye ameanza kujipanga kuingia kwenye vita ya kumwania Sanchez.
Sanchez ameifungia Arsenal mabao 17 kwenye ligi kuu tangu mwanzo wa msimu hadi hivi sasa.

Comments
Post a Comment