Usishangae Lwandamina akifungashiwa Virago vyake.


Klabu ya Yanga iliamua kumpiga chini kocha Hans der Pluijm na kuamua kumleta kocha George Lwandamina, lakini tangu kutua kwa kocha huyo hali imezidi kuwa mbaya kikosini.

Sababu zifuatazo zinaweza kumuondoa Lwandamina kwenye timu hiyo, licha ya kuwa na muda mfupi na kikosi hicho.

1. Muunganiko mbaya Kikosini.

Hadi sasa Kocha wa Yanga George Lwandamina ameshindwa kuamua watu sahihi wa kuunda kikosi imara cha timu, ni Simon Msuva, Obrey Chirwa na Thaban ndiyo wenye kuonekana kuwa imara ndani ya kikosi hicho.

Lwandamina ameshindwa kuwa na XI (first eleven) sahihi, hajaamua kati ya Deus Kaseke, Geoffrey Mwashiuya na Emanuel Martin nani atakuwa mkombozi katika upande wa kushoto, tumaini pekee n Simon Msuva ambaye hadi sasa ndiye aliyetengeneza mabao mengi zaidi ikiwemo na kufunga.

Kwa upande wa beki ya kati bado imekuwa kitendawili licha ya kutumainiwa kuwa bora kuliko Pluijm lakini kuipanga vema safu yake ya Ulinzi.

2. Uelekeo Mbaya wa kwenye ligi

Tangu kutua kwa George Lwandamina Yanga ameshindwa kuwa na mfululizo wa matokeo ya ushindi kama ilivyokuwa ndani misimu miwili iliyopita, licha kuwa nyuma kwa pointi mbili kwa watani wa jadi Simba bado Yanga haijakutana na Azam kwenye mechi ya marudiano endapo atapoteza mechi hiyo inaweza kutengeneza mazingira ya ubingwa kwa Simba.

3. Kufungwa na Simba

Licha ya Simba kuwa pungufu kwenye kwenye mtanange wa watani wa jadi lakini Yanga ilijikuta ikipoteza mechi hiyo kwa kufungwa mabao 2-1.

Simba ilionekana kutawala mpira na kuipa presha Yanga ambayo ilikuwa na wachezaji 11 uwanjani licha ya Bokungu kwenda nje kwa kadi nyekundu.

Ni wazi kocha kocha George Lwandamina aliishiwa mipango kwenye mechi hiyo.

4. Usajili wa Justice Zulu

Kiungo alikuwa chaguo la kwanza tangu kocha George Lwandamina alipotua Yanga. 

Mkata umeme huyo ambaye alishika umaarufu wa kutosha alipokuwa akitua nchini ameshindwa kuonesha thamani yake kutokana na kiwango kisichoridhisha hadi sasa.

Zulu amekuwa hakubaliki na mashabiki wa Yanga ambao wengi wao wamekuwa wakimkumbuka Mbuyu Twitte ambaye alitemwa kupisha usajili wa Zulu, hii inaweza kumpunguzia sifa kocha George Lwandamina.

5. Kufanya vibaya kwenye mashindano ya kimataifa

Msimu uliopita Yanga iliweza kufuzu kwenye hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika (Caf confederation cup), lakini kutua kwa George Lwandamina hajaweza kuonesha mabadiliko hayo kwenye michuano hali iliyopelekea Yanga kung'olewa kwenye raundi ya pili ya michuano ilipokutana na Zanaco.

6. Hakubaliki na mashabiki
Asilimia 90 ya mashabiki wa Yanga hawaridhishwi na mfumo wa sasa wa kocha wa sasa George Lwandamina na wengi wamekuwa wakimkumbuka Hans Pluijm hili linaweza kumuondoa Lwandamina kwenye timu hiyo.

7. Safu mbovu ya kiungo

Hadi sasa George Lwandamina ameshindwa kuwa safu imara ya kiungo hali inayochangia Yanga kufanya vibaya kwenye mashindano.

Kocha huyo ameonekana kujaribu kutumia mbinu mbadala ikiwemo kumtumia Kelvin Yondani kama namba 6 katika mechi dhidi ya Mtibwa na Zanaco.

Haruna Niyonzima ameonekana kuchoka na ameshindwa kufanya vizuri kuanzia mechi ya Simba, na Justice Zulu bado hajafanya makubwa kwenye timu hiyo.

Mechi yao dhidi ya Simba ilitoa taswira kamili ya muonekano wa eneo la kiungo la timu hiyo, hii ni sababu nyingine ambayo inaweza kumuondoa Lwandamina.

Comments