Vibarua viwili vya Azam FC kabla ya pasaka.


Timu ya Azam imeendelea kujifua katika uwanja wa Chamanzi Complex ikiwa ni sehemu ya kujipanga vizuri dhidi ya Yanga SC kwenye mchezo wa ligi kuu utakaopigwa kesho kwenye uwanja wa Taifa.

Pamoja na jitihada za kuikabiri Yanga bado Azam itakuwa ina kibarua kizito cha kuivaa Ndanda FC katika mchezo wa robo fainali ya kombe la Shirikisho.

Mbali na mchezo wa kesho Azam itashuka dimbani April 5 mwaka huu katika uwanja wa Chamanzi ili kusaka tiketi ya kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho.

Hadi sasa ni Simba na Mbao FC pekee ndiyo zilizojihakikishia kutinga nusu fainali ya michuano hiyo baada ya kutoka na matokeo ya ushindi.

Simba iliweza kuindoa Madini FC baada ya ushindi wa bao 1-0, na Mbao FC iliiondoa Kagera Sugar baada ya kuichapa bao 2-1 katika uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.

Comments