Yanga ndiyo basi tena, Zanaco apeta.


Mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara Yanga SC wameshindwa kutinga kwenye hatua ya makundi ya kombe la mabingwa barani Afrika.

Yanga iliruhusu Zanaco kupata bao la ugenini baada ya matokeo kuwa 1-1 kwenye mechi ya kwanza ambapo Yanga walikuwa wenyeji wa wazambia hao.

Msimu uliopita Yanga chini kocha Hans der Pluijm iliweza kutinga kwenye hatua ya makundi ya michuano hiyo ambapo ilimenyana na TP Mazembe, Mo Bejaia pamoja na Medeama.

Sare ya isiyokuwa na magoli dhidi ya Zanaco ndiyo iliyowaondoa Yanga kwenye kwenye raundi ya mpili ya mtoano kwenye ligi hiyo.

Comments