Mambo huenda yakawa si mambo kwa timu Yanga baada ya kupangiwa MC Alger FC ya Algeria katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika.
Yanga iling'olewa na Zanaco na sasa imeangukia kwa wababe hao wa Algeria kwenye raundi ya mtoano ikiwa ni sehemu muhimu ya kusaka tiketi ya kuingia kwenye hatua ya makundi.
MC Alger inashika nafasi ya 4 kwenye msimamo wa ligi kuu Algeria ikiwa na michezo 3 mkononi na huenda ikarejea kileleni endapo itashinda viporo hivyo.
Mwaka jana Yanga ilifanikiwa kutinga kwenye hatua ya Makundi hata hivyo ilishindwa kufuzu kuelekea hatua ya nusu fainali.
Comments
Post a Comment