Mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara Yanga SC wamesema kuwa hakuna timu itakayokwepa kipigo mbele yao.
Yanga itashuka dimbani leo dhidi ya Kiluvya katika mchezo wa kombe la shirikisho ili kuwania kutinga katika hatua ya robo fainali ya mashindano hayo.
Chanzo kilisema kuwa licha ya ratiba ngumu waliyonayo mbele yao lakini wamejipanga vema kushinda kila mechi.
" Hakuna mechi ndogo mbele yetu, kila mechi ni muhimu na ni lazima tushinde.
"Tunacheza dhidi ya Kiluvya leo nadhani ni lazma tushinde, tumejipanga pia ligi kuu kutetea ubingwa wetu." Kilisema chanzo hicho.

Comments
Post a Comment