Arsenal, Man utd zatupwa Europa ligi.


Wachambuzi wa kituo cha Skysports wameitoa timu ya Arsenal na Manchester United kwenye nne bora ya kufuzu ligi ya Mabingwa barani Ulaya.

Katika orodha ya wachambuzi hao akiwemo Gary Neville, Naill Quinn, Jamie Carragher, Thierry Henry na Graeme Souness wote kwa pamoja wamezitoa Man utd na Arsenal.

Jamie Carragher na Gary Neville wana amani kuwa Chelsea ndiye atakayekuwa bingwa akifuatiwa na Tottenham, Liverpool na Manchester city.

Lakini kwa upande wa Thierry Henry mtazamo wake ni tofauti na ule Gary Neville pamoja na Carragher yeye anaamini kuwa Chelsea atakuwa bingwa, ikifuatiwa na Tottenham, Manchester City na Liverpool akilingana mtazamo na Graeme Souness.

Kwa pamoja waamini huenda Manchester United atashiriki ligi ya mabingwa kwa kuwa ana nafasi kubwa ya kutwaa kombe la Europa ligi.

Comments