April 18, 2017
Waswahili husema mcheza kwao hutuzwa lakini haipo hivyo kwa upande wa Azam FC ambayo imafanya kitu tofauti msimu huu.
Azam imefanya vizuri kwenye mechi za ugenini kuliko nyumbani ikiwa imevuna asilimia 55 ya ushindi katika mechi zote alizocheza nje ya chamanzi Complex.
Hadi sasa Azam FC imeshinda mechi 6, imepata sare 5 na kupoteza mechi kwenye ilizopiga ugenini ikiwa na jumla ya pointi 23.
Mbali na takwimu hizo kwa ujumla kwa upande wa ugenini, lakini pia washambuliaji wa Azam akiwemo kinda wao Shaban Idd pamona na John Bocco wamefunga zaidi ugenini.
Shabaan Idd amefanya amefanya hivyo mara 4 kati ya goli 8 alizofunga kwenye mashindano yote msimu na Bocco amefunga mabao 3 ugenini.
Takwimu zimeonesha Azam ilikuwa hatari zaidi msimu huu kwa upande wa ugenini tofauti na ile michezo iliyotangwa katika dimba la Chamanzi Complex.
Source: www.azamfc.co.tz.

Comments
Post a Comment