Mabingwa wa kombe la Mapinduzi Azam FC leo watashuka dimbani katika mchezo wa kujipima nguvu dhidi ya African Lyon kwenye uwanja wa Chamanzi Complex majira ya saa 1.00 za usiku.
Benchi la ufundi la timu ya Azam imeandaa mchezo huo ikiwa ni sehemu ya kupima nguvu kikosi baada ya kukosa mechi ya ushindani ndani ya wiki hii.
Pia mchezo huo ni sehemu ya maandalizi kwa Azam FC ambayo kuanzia April 28 mwaka huu inatarajia mchezo wa nusu fainali kati ya Simba, Mbao, Yanga au Prisons katika michuano ya Azam Sports Federation Cup.
Mbali na mchezo, Mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara Yanga SC watachezo mchezo wa nusu wa nusu fainali ya michuano hiyo Dhidi ya Tanzania Prisons kutoka Mbeya.

Comments
Post a Comment