Azam yatinga nusu fainali FA.


Mabingwa wa kombe la Mapinduzi Azam FC wamefanikiwa kutinga nusu fainali ya kombe la shirikisho baada ya kuitwanga Ndanda bao 3-1 katika uwanja wa Chamanzi Complex.

Mshambuliaji kinda ambaye anachipukia kwenye kikosi cha Azam kwa sasa Shaban Idd alifunga mabao 2, na lingine la 3 likiwekwa nyavuni na Ramadhan Singano 'Messi'.

Azam imeungana na Simba pamoja na Mbao ambazo zilishatinga nusu fainali na sasa wanasubiri matokeo kati ya Yanga na Prisons ambao watacheza kesho.

Comments