Banda ruksa uwanjani.


April 21, 2017

Baada ya kukosa mechi mbili hatimaye beki wa Simba Abdi Banda amemaliza adhabu na hivyo atarejea uwanjani kumalizia mechi zilizobaki.

Banda alisimamishwa kutokana na utovu wa nidhamu aliotenda baada ya kumtwanga ngumi beki wa Kagera George Kavila katika mechi iliyochezwa kaitaba mkoani Kagera.

Mchezaji huyo atamalizia michezo mitatu ya mwisho ambayo Simba itacheza katika uwanja wa taifa dhidi ya African Lyon, Stand United na Mwadui FC.

Banda amekuwa mchezaji muhimu kwa upande wa Simba kutokana na uwezo wake mkubwa wa kucheza kwenye nafasi tofauti uwanjani.

Comments