Kocha wa zamani wa Liverpool na Real Madrid Rafael Benitez ameirejesha Newcastle ligi kuu baada ya ushindi wa jana dhidi ya Preston North End.
Newcastle ilipata ushindi wa bao 4-1 dhidi ya Preston North End hapo jana na kujihakikishia nafasi ya kurejea ligi kuu baada ya kukusanya jumla ya pointi 88.
Newcastle inashika nafasi ya pili chini ya Brightone Hove and Albion yenye pointi 92 zote kwa pamoja zikiwa zimecheza jumla ya michezo 44.
Ligi hiyo imebakiza michezo miwili kufikia tamati na wala hakuna dalili kwa timu zilizo chini timu hizo ikiwemo Reading yenye pointi 79 kuwafikia vinara hao.
Ni mwaka pekee umepita tangu Newcastle iliposhuka daraja na Benitez ameweza kuirejesha kwa mara nyingine.

Comments
Post a Comment