Bodi ya Arsenal yajiandaa kumjadili Wenger.


Bodi ya timu ya Arsenal inajindaa kukutana mwezi ujao ili kujadili hatma ya kocha wa sasa Arsene Wenger.

Bodi hiyo itawakutanisha washika dau wote ambao wanaisimamia Arsenal akiwemo Stan Kroenke ambaye ndiye mwenye asilimia kubwa katika hisa za timu hiyo.

Ingawa Wenger hajazumgumzia suala kuongeza mkataba au kuondoka lakini bodi hiyo itajadili mwenendo mzima wa timu ikiwemo kumpa mkataba mpya kocha huyo au kumuonesha mlango wa kutokea.

Comments