Can: Tumerudi kwenye ubora wetu


Kiungo wa Liverpool Emre Can amesema kuwa timu hiyo imeanza kurejea kwenye ubora wake kama ilivyokuwa hapo awali.

Liverpool iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Everton katika uwanja wa Anfiled hapo jana huku Can akiwa kwenye kiwango cha hali ya juu.

"Siwezi kusema kuwa tumejihakikishia nne bora kupitia matokeo haya, lakini tunaenda vizuri tunaweza kushiriki Champions ligi.

"Mwezi Desemba, January na February haukuwa mzuri kwetu lakini sasa tumerejea kwenye ubora wetu.

"Tunakiwa kufanya vizuri, nadhani tupo kwenye kiwango kizuri tunaweza kufikia malengo yetu." Alisema Can

Comments