Chelsea inahesabu hizi kuwa bingwa.


Timu ya Chelsea imeendelea kunusa harufu ya ubingwa ligi kuu England baadya kuichapa Everton bao 3-0 katika uwanja wa Goodson park hapo jana.

Ushindi umeingoza Chelsea kujizatiti katika mbio za ubingwa kwa tofauti ya pointi juu ya Tottenham ambayo jana ilipata ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Arsenal.

Mchezo wa jana unasadikika kuwa ndiyo mechi ngumu ya mwisho kwa timu hiyo ambayo imehitimisha mechi zote ngumu dhidi ya wababe wa England.

Chelsea ina kibarua cha kupata ushindi katika mechi za nne za mwisho zilizobaki dhidi ya West Brom, Middlesbrough, Watford na Sunderland.

Comments