Timu ya Chelsea imeendelea kulinda nafasi yake ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu baada ya kuichapa Southampton bao 4-2 katika uwanja wa Stamford Bridge.
Mabao ya Chelsea yalizamishwa nyavuni na Eden Hazard, Gary Cahil na Diego Costa aliyefunga mara mbili.
Kwa upande wa Southampton aliyekuwa kiungo wa zamani wa Chelsea Oriol Romeu na Ryan Bertrand ndiyo waliyoifungia timu hiyo.
Chelsea imejikita kileleni kwa pointi78 ikifuatiwa Tottenham Hotspurs yenye pointi 71 ikiwa na mchezo mmoja mkononi.

Comments
Post a Comment