Chelsea yatinga fainali kombe la FA.


April 22, 2017

Timu ya Chelsea imesonga kwenye hatua ya fainali ya kombe la FA baada ya kuichapa Tottenham bao 4-2 katika uwanja wa Wembley.

Mabao ya Chelsea yalifungwa na Willian aliyefunga mara 2, Eden Hazard aliyetokea benchi kipindi cha pili na Nemanja Matic.

Kwa Upande wa Tottenham Hotspurs mabao yao yalifunga na mshambuliaji wa timu hiyo Harry Kane pamoja Delle Ali.

Chelsea inamsubiri mshindi kati ya Arsenal na Manchester city watakaocheza kesho nusu ya pili katika mchezo wa fainali utakaopigwa Mei 27 mwaka huu katika uwanja wa Wembley.

Comments