Conte aingia mtegoni kuchagua nyota wa msimu.


April 14, 2017

Kocha wa Chelsea Antonio Conte amesema kuwa wachezaji wake wawili waliochaguliwa kuingia kwenye tuzo za mwaka za PFA wote ni bora ni kwa upande wake.

Mshambuliaji wa timu hiyo Eden Hazard pamoja na N'golo Kante wote wameingia kwenye kinyang'anyiro hicho wakiambata na Harry Kane, Alexis Sanchez na Romelu Lukaku.

Conte alisema kuwa ni jambo linalofurahisha kuona nyota hao wameingia pamoja kwenye kinyang'anyiro hicho.

"Ni jambo jema na la kupendeza kuona wachezaji wangu ni bora, nadhani tuzo ni muhimu na ubingwa ni muhimu zaidi." Alisema Conte.

Comments