CR7 si wa mchezo mchezo, atupia mbili Bayern ikifa Allianz Arena.


Mshambulaji nyota wa Real Madrid Christiano Ronaldo amedhihirisha kuwa yeye ni bora kwenye klabu hiyo baada ya kufunga bao 2 dhidi ya Bayern Munich.

Ronaldo alifunga bao hizo kwenye dakika ya 47 na 77 na kuifanya Real Madrid kuibuka kidedea kwa ushindi wa bao 2-1 katika mchezo wa kwanza wa robo fainali ya UCL.

Katika mechi hiyo Bayern Munich ilipata pigo baada ya beki wao Javier Martinez kuoneshwa kadi nyekundu katika dakika ya 61 ya mechi hiyo na kuifanya timu kucheza pungufu kwa dakika 30 za mwisho.

Comments