Mshambuliaji wa Real Madrid Christiano Ronaldo ameweka rekodi mpya kwenye ligi ya mabingwa barani Ulaya baada ya kufikisha idadi ya mabao 100 katika mechi 143 alizocheza kwenye ligi hiyo.
Ronaldo alifunga bao 2 jana katika ushindi waliopata dhidi ya Bayern Munich katika uwanja wa Allianz Arena nchini Ujermani.
Ronaldo anakuwa kinara wa mabao kwenye ligi na kumpiga chini mpinzani wake Lionel Messi ambaye ambaye amefunga mabao 97 katika mechi 118 alizocheza kwenye ligi hiyo.
Pia Ronaldo ameweza kuwafunika nyota wengine akiwemo Raul Gonzalez, Philipp Inzaghi na Gerd Muller.

Comments
Post a Comment