April 26, 2017
Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amesema milango ipo wazi kwa mlinda wa lango wa timu David De Gea endapo atahitaji kuondoka.
Hiyo ni habari njema kwa Real Madrid ambayo kwa muda imekuwa ikimfukuzia kipa huyo ili kupata golikipa atakayeziba nafasi ya Casillas ambaye alitimka FC Porto ya Ureno.
Raia huyo wa Hispania ni moja kati ya magoli kipa bora wanaotamba duniani kwa sasa.

Comments
Post a Comment