Genk ya Samatta yaondolewa Europa ligi.


April 21, 2017

Timu ya Genk imeshindwa kusonga mbele kwenye hatua ya nusu fainali ya kombe la Europa ligi baada ya kuong'olewa na Celta Vigo ya Hispania.

Genk ya Mbwana Samatta ilishindwa kupata matokeo ya ushindi katika uwanjani wa nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1.

Kwenye mchezo wa kwanza Genk ilikubali kipigo cha mabao 3-2 kwenye ardhi ya Hispania na ilikuwa ikihitaji bao moja pekee ili kutinga nusu fainali.

Celta Vigo imeungana na timu nyingine ikiwemo Man Utd, Olympic Lyon na Ajax kwenye hatua ya nusu fainali.

Comments