Gurdiola: Nimekuja England kuchukua mataji


Kocha wa Manchester city Pep Gurdiola amesema kuwa malengo yake ni kutwaa mataji katika timu hiyo badala ya kueneza falsafa yake.

Gurdiola alisema ni aibu kuzungumzia Falsafa ikiwa timu ipo kwenye mipango kutwaa kiwango kikubwa cha mataji na kujenga heshima.

"Falsafa si kitu cha msingi, mataji yanapewa nafasi kwanza.

"Lengo langu katika timu hii ni kubeba mataji na si kueneza falsafa yangu." Alisema Gurdiola

Comments