Mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard amefunga mabao mawili katika ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Manchester city katika uwanja wa Stamford Bridge.
Hazard alifunga bao hizo katika dakika ya 10 na ya 35 ya mechi na kuingoza Chelsea katika mbio za ubingwa ikiwa mbele kwa pointi 7 dhidi ya Tottenham.
Manchester city imekubali kuacha pointi 6 kwa Chelsea baada ya kuchapika nje ndani katika mechi ya nyumbani na ugenini walipokutana msimu huu.
Katika mechi ya kwanza Chelsea ilitoa dozi ya bao 3-1 kwa Man city ambayo ilikuwa katika uwanja wa Etihad.

Comments
Post a Comment