April 27, 2017.
Kiungo wa timu ya Azam Himid Mao 'Ninja' amesema kuwa wachezaji wa timu wana morali kuelekea mchezo wa nusu fainali dhidi ya Simba SC.
Himid alisema kuwa hali na nguvu ya mazoezi imeongezeka kwa wachezaji na wanmmejiwekea malengo ya kupata ushindi ili kutinga fainali ya kombe la FA.
"Tuna morali sana na mechi hiyo, hali ya mazoezi imekuwa juu kwa wachezaji hivyo tuna imani ya kupata ushindi.
" Siwezi kusema Simba si wazuri, lakini tumeweka nia na lengo la ushindi." Alisema kiungo huyo
Simba na Azam zitakutana katika nusu ya kwanza ya kombe la FA katika mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa jumamosi ya wiki hii.
Source-azam.co.tz
Source-azam.co.tz

Comments
Post a Comment