Ibrahimovic akataa mkataba mpya Man Utd.


April 27, 2017

Mshambuliaji wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic amekataa kupokea ofa ya mkataba mpya kwa msimu mwingine ndani ya timu hiyo.

Kocha wa timu hiyo Jose Mourinho ameadhimia kumwongeza mwaka mmoja strika huyo licha ya majeraha ya goti yatakayomuweka nje kwa muda mrefu.

Raia huyo wa Sweden aliumia katika mchezo wa robo fainali wa michuano ya Europa ligi dhidi ya Anderlecht ya Ubelgiji.

Ibrahimovic ameifungia timu hiyo jumla ya mabao 28 katika mechi zote alizoichezea Man Utd msimu huu.

Comments