Timu ya Azam imeibuka na ushindi wa bao 2-0 katika mchezo wa kujipima nguvu dhidi ya African Lyon uliopigwa jana katika uwanja wa Chamanzi Complex.
Beki wa Azam FC Erasto Nyoni na kiungo wa timu Mudathir Yahya ndiyo waliyofunga mabao hayo muhimu katika mechi hiyo.
Mechi hiyo iliandaliwa na benchi la ufundi la Azam ulikuwa na lengo la kupima mwenendo wa kikosi hicho baada ya kukosekana kwa mechi ushindani ndani wiki hii.
Pia Azam ilitumia mchezo huo wa kirafiki ikiwa ni sehemu ya mikakati yao ya kujiandaa na nusu fainali ya kombe la FA ambayo itachezwa April 28 mwaka huu.

Comments
Post a Comment