Timu ya Juventus maarufu kama kibibi cha Turin imetinga nusu fainali kwenye michuano ya champions league baada ya kuindoa Barcelona.
Juventus ilipata ushindi wa mabao 3-0 katika mechi ya kwanza ikiwa nyumbani ambapo katika mchezo wa marudiano imekomaa na sare isiyokuwa na magoli katika uwanja wa Camp Nou.
Juventus imeungana na Real Madrid, Atletico Madrid na Monaco ambayo tayari wamefuzu kwenye hatua ya nusu fainali.

Comments
Post a Comment