Timu ya Juventus imeonesha kuwa ilikuwa sawa kuitaka Barcelona kwenye hatua ya robo fainali baada ya kukata kiu yao kwa kuifunga timu hiyo bao 3-0.
Mabao ya Juventus yalifungwa na Mshambuliaji Kinda Paulo Dybala aliyefunga mara mbili ndani ya dakika 10 za mechi hiyo na bao la tatu lilizamishwa wavuni na Giorginio Chiellini.
Hata hivyo bado Barcelona inayo nafasi ya kujiuliza katika mchezo wa marudiano katika uwanja wa Camp Nou utakaopigwa wiki mbili zijazo.

Comments
Post a Comment