Kamusoko aipa kibarua kizito MC Alger.


Kiungo wa Yanga Thaban Kamusoko ndiye aliyeifungia timu hiyo bao pekee la ushindi katika mchezo wa kimataifa dhidi ya MC Alger ya Algeria.

Kamosoko alifunga bao hilo kwenye dakika 60 ya mchezo huo baada ya kuunganisha pasi safi iliyotoka kwa Simon Msuva.

Kutokana na ushindi huo ambao timu ya Yanga imeupata katika uwanja wa nyumban, MC Alger itakuwa na kazi nzito ya kusaka ushindi unaoanzia bao 2-0 itakapokuw nyumbani.

Bao pekee la Kamusoko limetanguliza matumaini mapya kwa Yanga SC kuelekea katika mchezo wa marudiano dhidi ya mafundi hao wa Algeria.

Comments