Kane arejea uwanjani.


Mshambuliaji wa kimataifa wa England Harry Kane ameungana na wenzake kikosini baada ya kupona jeraha la enka.

Kane aliumia katika mchezo wa robo fainali ya kombe la FA dhidi ya Millwall Machi 12 mwaka huu.

Kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino alisema kuwa Kane atakuwa sehemu ya kikosi kitakachoshuka dimbani dhidi ya Watford.

"Nadhani nitaamua kesho kama Kane ataanza au atatokea benchi, lakini jambo jema kwa kuwa amerejea sasa.

"Yeye ni mchezaji muhimu siku zote na wakati wote katika kikosi cha timu." Alisema Pochettino

Comments