Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema kuwa ataridhika endapo timu yake itaingia kwenye nne bora msimu huu na kushiriki ligi ya mabingwa.
Mara ya mwisho timu hiyo kushiriki ligi ya mabingwa barani Ulaya ilikuwa mwaka 2014/15 ambapo Liverpool iliondolewa kwenye hatua ya makundi ikishika namba tatu chini ya Real Madrid na FC Basel.
"Nitaridhika endapo timu yangu itaingia nne bora na kushiriki ligi ya mabingwa.
" kuna presha kubwa, kila mechi ni ngumu na ina presha kubwa. Lakini malengo yangu ni kuiona Liverpool inaingia kwenye ligi ya mabingwa barani Ulaya." Alisema Klopp.
Comments
Post a Comment