Kocha wa sasa wa Liverpool Jurgen Klopp amesema kuwa haishangazi endapo atamaliza rasmi kazi yake ya ukocha akiwa na timu hiyo.
Raia huyo wa Ujermani alisaini miaka 6 ya kuendelea kuiona Liverpool na kuweka mipango mingi ikiwemo kuibua vipaji ambavyo vitasapoti kikosi cha timu hiyo.
"Kama nitatimiza vema makubaliano ya mkataba wangu basi bila shaka nitabaki hapa kwa miaka mingi sana.
"Watu wengi wanategemea Liverpool itatwaa mataji, nadhani kuna taji litapatikana hapa katika kipindi changu. Nina imani nitamaliza maisha yangu ya soka katika timu hii." alisema Klopp.

Comments
Post a Comment