April 28, 2017
Nyota wa Liverpool Adam Lallana na Daniel Sturridge wameanza mazoezi baada ya kutoka kwenye majeraha na wataongeza nguvu katika mechi dhidi ya Watford.
Sturridge alikosa mechi ya Crystal Palace lakini Adam Lallana amekuwa nje uwanja tangu March 19 alipoumia wakati akiitumikia timu ya taifa.
Kurejea kwa wachezaji hao kutaongeza nguvu kwenye kikosi cha Liverpool ambacho kinapigania nafasi ya kushiriki ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Comments
Post a Comment