Walichemka lakini leo wamekuwa lulu.

April 19, 2017
                          Kevin De bruyne

Raia huyu wa Ubelgiji alitokea katika timu ya Genk na kutua Chelsea mwaka 2012. 

Alipokuwa Chelsea aliweza kucheza mechi 3 pekee bila kufunga goli, hata hivyo aliyekuwa kocha wa Chelsea wakati huo Jose Mourinho hakuridhishwa na kiwango chake na hivyo alimpiga bei katika timu ya Wolfsburg.

Akiwa Wolfsburg De Bruyne alikuwa moto, aliweza kuifungia Wolfsburg mabao 13 na kuishawishi Manchester city kumnunua kwa mabilioni ya pesa, na sasa amekuwa moja ya mchezaji tegemezi ndani ya kikosi cha Manchester city.

                           Michael Keane

Beki huyu mwenye miaka 23 aliwahi kuichezea Manchester united kwenye timu ya vijana mwaka 2011 hadi 2015 ambapo walimtoa kwa mkopo kwenda Leicester, Derby country na Burnley ambayo ilimsajili moja kwa moja nyota huyo.

Keane amekuwa bora na muhimili katika kikosi cha Burnley ambacho kinaonekana kuwa na ukuta imara unaotokana na umakini Muingereza huyo. Makocha mbali mbali akiwemo Jose Mourinho, Jurgen Klopp na Antonio Conte wameanza kumtolea macho nyota huyo.

                               Iago Aspas

Mshambuliaji huyu alisajiliwa na Liverpool akitokea Celta Vigo ya Hispani chini ya Brendan Rodgers mwaka 2013. Aspas alishindwa kuwika Liverpool kutokana na uwezo wa Daniel Sturridge na Luis Suarez.

Baadae alirejea Hispania ambapo alitua Sevilla kwa mkopo na kurejea tena Celta Vigo. Aspas amekuwa mshambuliaji tegemeo kutokana na uwezo wake mkubwa wa kufumania nyavu na kuingia katika orodha ya wafungaji wanaotamba katika ligi ya Hispania.

                           Marcos Alonso

Unaweza kushangazwa na Alonso na kumjumuisha katika moja ya nyota ambayo wamewahi kutamba kwenye soka kabla ya kutua Stamford Bridge.

Nyota huyu alitokea Real Madrid mwaka 2010 na kutua Bolton ya Uingereza, lakini hata hivyo aliuzwa kwenda Fiorentina ambayo baadae ilimtoa kwa mkopo na 

Sunderland na kumrejesha tena Fiorentina.
Inawezekana dunia ilistuka wakati Antonio Conte alipoamua kutoa Kiasi cha £20 milioni na kumsajili nyota huyo. Alonso amekuwa mchezaji bora katika kikosi cha Chelsea na kujizolea umaarufu msimu huu. 

Anafiti vizuri katika mfumo 3-4-3 unaotumiwa na Antonio Conte.

                           Romelu Lukaku

Romelu Lukaku aliwahi kuichezea Chelsea tangu 2011 hadi 2015. Aliwahi kucheza West Brom kwa mkopo na baadae alichukuliwa na Everton ambayo iliamua kumsajili moja kwa moja.

Hakuna ubishi juu ya kipaji na ubora wa mbelgiji huyo ambaye ni hatari kwenye lango la goli. Lukaku amefunga jumla ya mabao 24 kwenye ligi ya England msimu na kuongoza kwenye orodha ya wafungaji wa ligi hiyo.

Uwezo na kipaji chake unawatoa macho makocha kadhaa barani Ulaya akiwemo Jose Mourinho na Antonio Conte ambaye tayari amewasilisha jina la nyota kwenye orodha ya wachezaji anaotegemea kuwasajili.

Comments